Ijumaa , 16th Mei , 2014

Uongozi wa tawi la Yanga la Tandale Mtogole umesema tawi hiklo halijafutwa kwa sababu jambo lililosemwa na tawi hilo ni la ukweli na kumwomba msaada Mosha aiokoe Yanga.

Siku chache baada ya uongozi wa klabu ya Yanga kulifuta tawi la Tandale kwa mtogole jijini Dar es salaam na kufungia baadhi ya wanachama wa timu hiyo, hii leo uongozi wa tawi hilo lenye ushawishi mkubwa kwa wanachama wa yanga umesema kamwe hautambui kufutwa kwa tawi hilo

Akiongea kwa kujiamini msemaji wa tawi hilo Salum Bilali amesema kitendo cha wao kuukosoa uongozi na kusema ukweli juu ya matatizo ya klabu yao ndiyo chanzo cha tawi lao kutangazwa kufutwa kitu ambacho hawakiafiki kwakuwa ni kinyume na katiba ya klabu hiyo.