Jumanne , 30th Jan , 2024

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Gerson Msigwa amesema timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inarejea nchini kwa awamu,

“Kuna changamoto kidogo ya usafiri. Hatukufanikiwa kupata tiketi za timu nzima kwa mara moja kwahiyo walioanza kuwasili nchini jana ni wachezaji na viongozi 15.”

“Kuna baadhi yao watafika leo wengine kesho. Pia kuna wachezaji ambao wamerejea moja kwa moja kwenye nchi ambako timu zao wanazochezea” Katibu  Gerson Msigwa.

Taifa Stars ilitupwa nje ya Fainali za kombe la Mataifa Afrika na kuondoka na alama 2 katika kundi F ambazo zilikuwa na timu ya Morrocco,Zambia ,DRC na Tanzania