Taarifa rasmi kutoka TPLB kuhusu Simba na Namungo

Jumatano , 18th Nov , 2020

Bodi ya Ligi imefanya mabadiliko ya ratiba ya mechi za Simba na Namungo Fc kutokana na timu hizo kukabiliwa na majukumu ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano iliyochini ya Shirikisho la mpira wa miguu Afrika 'CAF'.

Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Meddie Kagere akikatiza katikati ya wachezaji wa Namungo katika moja ya mechi ya VPL msimu uliopita.

Mchezo kati ya Dodoma Jiji dhidi ya Simba uliokuwa upigwa Novemba 24 umesogewa mbele ili kuwapa nafasi wekundu wa msimbazi kujiandaa na mchezo wa hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Plateau United.

Jumamosi Novemba 21 Simba itacheza na Coastal Union mkoani Arusha kabla ya safari ya kuelekea nchini Nigeria kuikabili Plateau United kwenye mchezo ambao utapigwa mwishoni mwa mwezi huu

Namungo wao walipaswa kucheza na KMC Novemba 24, nao mchezo wao umesogezwa mbele wapate nafasi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya wapinzani wao wa michuano ya kombe la Shirikisho kutoka Sudan Kusini.