Jumatatu , 18th Jul , 2022

Timu ya Tanzania “Taifa Stars” inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Sudan Kusini mnamo Julai 19 , 2022 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya kufuzu kwa fainali za michuano ya CHAN 2023.

Taifa Stars

Kocha mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen amesema maandalizi ya kikosi chake yanakweda vyema huku lengo la mchezo huo wa kirafiki ni kuangalia kikosi chake kabla ya kucheza na Somalia mnamo Julai 23 na 30, 2022 kwenye dimba la Benjamin Mkapa kwenye michezo ya kufuzu CHAN 2023 .

''Kesho tunacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Sudani kusini asubuhi nanitatumia wachezaji wote nilikuwa kwenye kikosi changu kabla ya michezo ya CHAN huku malengo yetu ni kupata ushindi ili tujiweke katika mazingira mazuri'' Kim Paulsen Kocha Stars.

Katika hatua nyingine,Golikipa wa Taifa Stars Aishi Manula amesema morali ni kubwa kuelekea kwenye michezo ya kufuzu kwa mashindano hayo huku akisifia maingizo mapya ya wachezaji walioitwa katika kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa na michuano ya Chan.

Taifa Stars imeingia kambini tangu Julai 15 kujiandaa na michezo miwili ya kufuzu kwa fainali za michuano ya CHAN 2023 dhidi ya Somalia huku tayari nyota 24 walioitwa wakiwa wameripoti kambini na kuendelea na mazoezi na kikosi hicho