Ijumaa , 15th Dec , 2023

Golikipa wa Singida Fountain Gate Beno Kakolanya amefungiwa kutocheza michezo 3 na faini ya Shilingi Milioni moja (1,000,000) na bodi ya usimamizi na uendeshaji wa Ligi TPLB kwa makosa ya kutoa Lugha ya matusi na kujaribu kumshambuliaji kwa ngumi kiongozi wa Coastal Union Juma Kindo.

Golikipa wa Singida FG amefungiwa michezo 3 na faini ya shilingi milioni 1 kwa kosa la kuwafanyia vurugu Coastal Union

Kakolanya alifanya makosa hayo baada ya kikosi cha Singida FG kuvamia mazoezi ya Coastal Union na kusababisha vurugu siku moja kabla ya mchezo wa Ligi kuu mchezo ambao Coastal walienda kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1 kwenye uwanja wa Liti.

Vurugu hizo zilitokea baada ya basi la Singida Fountain Gate likiwa na wachezaji na viongozi wa benchi la Ufundi kuingia kwenye uwanja wa Liti ambapo ilikuwa ni siku moja kabla ya mchezo kikanuni Coastal Union walikuwa na haki ya kuutumia uwanja huo.

Kufutia kitendo hicho klabu ya Singida FG imepigwa faini ya shilingi million 1(1,000,000) na kocha msaidizi wa kikosi hicho Thabo Krause amepigwa faini ya shilingi milioni 1 na kafungiwa michezo 3,

Huku Wachezaji Deus Kaseke na Hamadi Waziri wote wamepigwa faini ya shilingi laki tano (500,000) kila mmoja kwa kushiriki kwenye vurugu hizo.