Jumapili , 23rd Apr , 2017

Mwanariadha pekee wa Tanzania Alphonce Felix Simbu, leo Jumapili ataibeba bendera ya Tanzania kwenye  mashindano ya London Marathon yanayofanyika jijini London. 

Alphonce Felix Simbu

Alphonce, ambaye ni Mtanzania wa kwanza kushinda medali ya dhahabu katika mashindano maarufu ya Standard Chartered Mumbai Marathon, anatarajiwa kuwapa wakati mgumu manguli wa riadha ulimwenguni wanaoshiriki mbio hizo za London akiwemo Muethiopia Kenenisa Bekela pamoja na wengine kutoka Ethiopia na Kenya.

“Nitapambana kwa nguvu zangu zote...nina imani nitashinda kwani nimefanya mazoezi ya kutosha na nina ari na moyo wa kushinda. Naomba sala za watanzania wote ili niweze kuleta medali nyumbani” amesema Simbu

Tumtakie kila la kheri