Simba yakamatwa na Azam FC, Chama akosa penati

Jumapili , 7th Feb , 2021

Mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara kati ya Simba SC dhidi ya Azam FC umemalizika kwa sare ya 1-1, baada ya timu zote mbili kucheza kwa kushambuliana kwa kasi hususani kwa kupeana vipindi.

Wachezaji wa Azam FC wakishangilia goli la kwanza

Simba walitangulia kwa goli la kipindi cha kwanza kutoka kwa Meddie Kagere dakika ya 38, ambalo lilidumu hadi mapumziko kabla ya Azam FC kurejea na kutawala mchezo.

Goli la kwanza la Simba SC kupitia kwa Meddie Kagere

Kipindi cha pili Azam FC waliwaingiza Mudathir Yahya na Yahya Zayd ambao walibadilisha mchezo na kupelekea Azam FC kupata goli la kusawazisha dakika ya 67 kupitia kwa Idd Selemani na baadaye dakika ya 76 kuongeza goli la pili kupitia kwa Ayoub Lyanga.

Goli la pili la Simba kutoka kwa Luis Miquissone

Simba walisawazisha dakika ya 78 kupitia kwa Luis Miquissone, hivyo kufanya mchezo umalizike kwa sare ya 2-2.

Goli la pili la Azam FC kupitia kwa Ayoub Lyanga

Simba wamefikisha pointi 39 wakiendelea kubaki kwenye nafasi ya pili huku Azam FC wakifikisha pointi 33 katika nafasi ya tatu.