Simba SC yaifunga Al Ahly na kuongoza Kundi A

Jumanne , 23rd Feb , 2021

Klabu ya soka ya Simba imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Al Ahly ya Misri kwenye mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Afrika, uliopigwa jioni ya leo Februari 23 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Miquissone akishangilia goli dhidi ya Al Ahly

Goli pekee la Simba SC kwenye mchezo huo limefungwa na winga Luis Miquissone dakika ya 32 baada ya kupiga shuti kali.

Ushindi huo umeifanya Simba SC kuongoza Kundi A baada ya kufikisha pointi 6 kwenye michezo miwili ya kwanza.

Nafasi ya pili inashikiliwa na Al Ahly yenye pointi 3, nafasi ya tatu ni AS Vita yenye pointi tatu baada ya kupata ushindi wa goli 4-1 dhidi ya Al Merrick.