Alhamisi , 13th Jan , 2022

Michuano ya Kombe la Mapinduzi inataraji kuhitimishwa leo kwa mchezo mmoja wa fainali ambao utawakutanisha Mabingwa wa Kihistoria wa Kombe hilo, Klabu ya Azam dhidi ya Makamu Bingwa , Klabu ya Simba saa 2:15 usiku wa leo.

(Kikosi cha Simba SC (Juu), kikosi cha Azam FC (Chini) kwa msimu 2021-22)

Kuelekea kwenye mchezo huo unaotaraji kuchezwa kwenye dimba la Amani Visiwani Zanzibara, Kocha wa Azam FC, Abdihamin Mohammed Moallin amekiri Simba ni timu nzuri lakini hawana budi kucheza kwa nidhamu ili kupata ushindi.

"Utakuwa mchezo wa ushindani, tunaenda kupambana kutafuta matokeo mazuri ili kufikia malengo yetu. Simba ni timu nzuri lakini tunaenda kucheza kwa tahadhari kubwa ili kupata ushindi" Amesema Moallin kocha kutoka Somalia.

Kwa Upande wa Kocha wa Simba SC, Pablo Franco Martin amesema lengo la kwanza la Wekundu wa Msimbazi lilikuwa ni kufika fainali lakini kwa sasa ni muda wa kubeba komb hilo kwa ajili ya Wanasimba wote.

"Azam ina wachezaji wazuri na wanapambana kutafuta matokeo. tumeona ubora  waonna kuufanyia kazi. Tuna waheshimu, tutacheza kwa tahadhari ili kufikia malengo yanayotarajiwana wana Simba Wote".

"Lengo letu la kwanza lilikuwa kufika fainali, hilo tumefanikiwa na sasa ni kutwaa ubingwa. Nawapongeza wapinzani wetu pia kufika hatua hii. Naamini itakuwa mechi ngumu pande zote mbili". Amesema Pablo.

Mchezo huo unatazamiwa kuwa wa Kisasi kwa Simba SC, Kwani wameshapoteza fainali mbili mbele ya Matajiri hao wa Jiji la Dar es Salaam klabu ya Azam. Mbali na tambo hizo Makocha wote wamethibitisha kuwa wachezaji wote wako fiti na tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao pia ni wa kisasi kwa Upande wa Azam baada yakufungwa 2-1 na Simba SCkwenye Ligi kuu NBA Tanzania Disemba mwishino mwaka 2021.