Simba kufuta uteja kwenye ardhi ya Misri

Jumanne , 6th Apr , 2021

Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika Simba Sc, wataondoka nchini leo Saa 9:25 Alasiri kueleka nchini Misri tayari kwa maandalizi ya mchezo dhidi ya Al Ahly utakao chezwa Aprili 9, 2021.

Wachezaji wa Simba SC

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo juu ya safari hiyo imesema,

‘’Kikosi cha wawakilishi wa nchi kimataifa leo jumanne Aprili 6, 2021 saa 9:25 alasiri kitaondoka nchini kwenda Misri kwa kupitia Dubai. Kitaondoka Dar mpaka Dubai, kitapumzika hapo na jumatano asubuhi kitaondoka Dubai kwenda Cairo na kufika saa 4:05 asubuhi.’’

huu ni mchezo wa kukamilisha ratiba kwani kimahesabu, Simba na Al Ahly zimefuzu hatua ya robo fainali kutoka kundi A’ na Simba ndio vinara wa kundi hilo wakiongoza kundi kwa tofauti ya alama 5 wakiwa na alama 13, wakati Al Ahly wapo nafasi ya pili wakiwa na alama 8, nafasi ya tatu wapo AS Vital wakiwa na alama 4 na AL Merrikh wanaburuza mkia kwenye kundi hilo wakiwa na alama 2.

Katika michezo 3 ya mwisho timu hizi kukutana Simba imeshinda mara mbili na imefungwa mchezo mmoja, lakini michezo yote imeshinda nyumbani, na mchezo wa mwisho waliocheza Misri wenyeji AL Ahly waliiny uka Simba mabao 5-0 mwaka 2019.