Jumanne , 29th Sep , 2020

Mkurungenzi wa michezo Tanzania, Yusuph Singo amesema Serikali haitavumilia tena vitendo vinavyo endelea kwa baadhi ya mashabiki viwanjani na watawachukulia hatua bila kujali ni wa timu gani.

Mkurugenzi wa Michezo Yusuph Singo akizungumza na EATV juu ya vurugu za mashabiki viwanjani.

Kauli hiyo inakuja siku mbili baada ya baadhi ya mashabiki wa Yanga kuwapiga mashabiki wa Simba katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Yanga.

''Kumekuwa na utani wa jadi baina na Simba na Yanga lakini wanako elekea ni uadui na uhasama kitu ambacho Serikali haiwezi kufumbia macho swala hilo, ndiyo maana yoyote atayebainika amefanya tukio hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake'' Singo amesema.

Singo ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya tano chini Rais John Magufuli ina hamasisha kuhusu suala la amani na upendo hivyo anashangazwa kuona watu wanapigana viwanjani hivyo amewataka TFF na Bodi ya Ligi kuchukuaa hatua kali endapo matukio kama haya yataendelea.

Aidha Singo amewataka viongozi na wasemaji wa klabu hizo kuacha kutumia lugha zisizofaa ambazo wakati mwingine zinapelekea mashabiki kupaniki na kufanya fujo.