Ijumaa , 1st Dec , 2023

Aliyewahi kuwa mchezaji wa zamani wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa uingereza James Lee Duncan Carragher kwenye mazungumzo yake na kituo cha ''CBS sport'' aligusiwa kuhusu uwezo wa miamba wawili kwenye ulimwengu wa mpira Messi na Ronaldo

 

Mtazamo wa James Carragher ulionesha wazi kukubaliana na kiwango na ubora wa mchezaji wa klabu ya Inter Miami Lionel Messi ukimlinganisha na Ronaldo.

''Kuhusu nani bora kati ya Messi na Ronaldo haujawahi kuwa mjadala, hakuna namna Ronaldo amefikia ubora wa Lionel Messi, Ronaldo ni miongoni mwa wafungaji bora wa muda wate lakini Messi ni mchezaji bora wa muda wote'' - James Lee Duncan Carragher