Jumanne , 6th Apr , 2021

Ligi ya mabingwa barani ulaya hatua ya robo fainali itaanza kutimua vumbi leo usiku ambapo itachezwa michezo miwili, nchini Hispania na England.

Mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus

Vinara wa ligi kuu England Manchester City watakuwa wenyeji wa Borussia Dortmunda ya Ujerumani mchezo utakao chezwa kwenye dimba la Etihad. Manchester City wamefika hatua hii ya robo fainali kwa mara ya 4 mfululizo na katika misimu 3 mfululizo iliyopita wameishia kwenye hatua hii wameshindwa kwenda nusu fainali na wamefika hatua ya nusu fainali mara moja tu msimu wa 2015-16. wakati Dortmund hii ni kwa mara ya kwanza wanacheza robo fainali tangu mwaka 2017.

Mara ya mwisho timu hizi kukutana kwenye michuano hii ilikuwa kwenye hatua ya makundi msimu wa 2012-13, mchezo wa kwanza ulimalizika kwa sare ya bao 1-1, na mchezo wa pili ambao City walikuwa wenyeji Dortmund walishinda 1-0.

Nchini Hispania mabingwa wa kihistoria Real Madrid watakuwa wanaminyana na Liverpool ya England katika dimba la Alfredo Di Stefano. Timu hizi zinakutana kwa mara ya kwanza tangu zilipokutana kwenye mchezo wa fainali ya michuano hii mwaka 2018 mchezo amabao Real Madrid walishinda kwa mabao 3-1, hivyo mchezo wa usiku wa leo ni wakulipa kisasi kwa Liverpool.

Timu zote hazijawa kwenye kiwango bora cha uchezaji, na zimekumbwa sana na majeruhi kwa wachezaji wao muhimu. Madrid watamkosa nahodha Sergio Ramos kutokana na majeruhi lakini pia Raphael Varane ambaye ana maambukizi ya virusi vya Corona.

Kwa Liverpool hakuna mchezaji mwingine mwenye majeruhi zaidi ya wale ambao ni wana majeruhi ya muda mrefu ambao ni Jorda Henderson, Joe Gomez, Joel Matip na Virgil van Dijk.

Michezo yote hii inachezwa saa 4:00 usiku