Alhamisi , 25th Aug , 2016

Mabingwa watetezi wa michuano ya Mabingwa Ulaya Real Madrid imepangwa katika kundi moja na Borrusia Dortmund katika hatua ya makundi ya michuano hiyo msimu wa 2016/17.

Real Madrid baada ya kutwaa ubingwa wa Ulaya msimu wa 2015/16

Kwa upande wa wabaya wao Barcelona na Atletico Madrid, pia wana kibarua kizito kufuatia makundi yao kujumuisha vigogo wa soka barani Ulaya.

Kwa upande wa mabingwa wapya wa England Leicester City, wao wamepangwa kandi linaloonekana kuwa rahisi kidogo kutokana na kujazwa na timu za kawaida

Droo ya upangaji wa makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya msimu wa 2016/2017, imechezeshwa usiku huu, mjini Monaco nchini Ufaransa, ukishirisha jumla ya timu 32, kutoka nchi wanachama wa UEFA.

Droo hiyo imechezeshwa kulingana na kanuni za UEFA, ambapo timu za nchi moja au ukanda mmoja hazipaswi kuwa kwenye kundi moja, katika makundi 8 ya timu hizo 32.

Matokeo ya droo hiyo yako kama ifuatavyo:-
Kundi A: Paris Saint-Germain (FRA), Arsenal (ENG), Basel (SUI), Ludogorets Razgrad (BUL)

Kundi B: Benfica (POR), Napoli (ITA), Dynamo Kyiv (UKR), Beşiktaş (TUR)

Kundi C: Barcelona (ESP), Manchester City (ENG), Borussia Mönchengladbach (GER), Celtic (SCO)

Kundi D: Bayern München (GER), Atlético Madrid (ESP), PSV Eindhoven (NED), Rostov (RUS)

Kundi E: CSKA Moskva (RUS), Bayer Leverkusen (GER), Tottenham Hotspur (ENG), Monaco (FRA)

Kundi F: Real Madrid (ESP, holders), Borussia Dortmund (GER), Sporting CP (POR), Legia Warszawa (POL)

Kundi G: Leicester City (ENG), Porto (POR), Club Brugge (BEL), FC København (DEN)

Kundi H: Juventus (ITA), Sevilla (ESP), Lyon (FRA), Dinamo Zagreb (CRO)

Awali droo hiyo, iligawanywa katika vyungu vinne, vyenye timu 8 kila moja, ambapo Mabingwa wa Uingereza Leicester City, walikuwa chungu A na mabingwa wa Ulaya Real Madrid ya nchini Uhispania, na haikupaswa kukutana na vilabu vya Barcelona, Bayern Munich, Juventus, Benfica, Paris Saint-Germain na CSKA Moscow.

Michezo ya makundi ya ligi hiyo kubwa kabisa ya vilabu barani Ulaya, inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia septemba 13 na 14, mwaka huu.