Jumatano , 7th Apr , 2021

Klabu za Real Madrid na Manchester City jana zilipata ushindi katika michezo yake ya mkondo wa kwanza wa ligi ya mabingwa Ulaya iliyopo katika hatua ya robo finali, hivyo kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya nusu fainali.

Vinicius Junior chipukizi wa Real Madrid anayefanya vyema kwa sasa

Real Madrid wakiwa nyumbani walipata ushindi wa magoli 3-1 mabao yaliyofugwa na Mbrazil Vinicius Junior katika dakika za 27 na 64 huku goli jingine likifungwa na Marco Asensio dakika ya 35 , goli la Liverpool limefungwa na Mohamed Salah kunako dakika ya 50.

Manchester City wao walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Borussia Dortmund mechi iliyokuwa na ushindani mkubwa sana magoli yao yamefungwa na Kevin de Bruyne dakika ya 19 na Phil Foden 89 na lile la Dortmund limefungwa na Marco Reus 83.

Kwa matokeo hayo yana maana Zinedine Zidane na vijana wake ambao walikuwa kwenye nidhamu ya juu sana ya mchezo siku ya jana watalazimika kucheza kwa umakini mkubwa katika mechi ya mkondo wa pili ,utakaochezwa tarehe 14 /04/2021 ili waweze kufuzu hatua muhimu ya nusu fainali.

Kwa upande wa Pep Guardiola na vijana wake wao pia wanapaswa kuwa makini angalau kuandikisha historia ya kucheza hatua ya nusu fainali kwa miaka ya hivi karibuni pamoja na kuwa na timu bora hawajafanikiwa kucheza hatua hiyo, watarejeana na Dortmund tarehe 14/04/2021

leo robo fainali hizo zitaendelea kwa michezo miwili,ambapo bingwa mtetezi na makamu bingwa wa wa msimu wa 2019/20 Bayern Munich na PSG watakutana , huku Chelsea mabingwa wa msimu 2011/12 wataumana na mabingwa wa msimu wa 2003/04