Jumatatu , 23rd Nov , 2020

Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Ahmad Ahmad, amefungiwa miaka mitano na Shirikisho la soka Duniani (FIFA), kutojihusisha na soka.

Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Ahmad Ahmad

Sababu imeelezwa ni matumizi mabaya ya ofisi na pesa za CAF, ambapo Bw. Ahmad anadaiwa kujizawadia pamoja na kujipatia zawadi nyingine kwa jina la CAF.

Ahmad sasa atalazimika kuachia ofisi kabla ya uchaguzi mwezi Machi, 2021, ambapo alikuwa ametangaza nia ya kuwania awamu ya pili.

FIFA kupitia kamati yake ya maadili imeeleza kuwa imefanya uchunguzi wa kina na kujiridhisha huu ya hilo hivyo mbali na kufungiwa miaka mitano pia amepigwa faini ya shilingi za Tanzania zaidi ya milioni 500.