Alhamisi , 7th Dec , 2023

Kupitia Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk.Damas Ndumbaro amesema kuwa Rais Samia ameahidi kutoa bonus/zawadi ya shilingi Milioni 200 kwa timu ya taifa ya wanawake "Twiga Stars" mara baada ya kufanikiwa kukata tiketi ya kufuzu kucheza michuano WAFCON itakayofanyika Morocco 2024.

Waziri Dk.Ndumbaro ameyasema hayo wakati akiwa kwenye uwanja wa ndege wa J.K Nyerere kuipokea Timu ya Taifa ya Wanawake “Twiga Stars” ilipowasili ikitokea Togo kwenye mchezo wa marudiano kufuzu WAFCON.