Raiola ajibia kuhusu kupokea malipo ya Haaland

Jumatatu , 5th Apr , 2021

Wakala wa mchezaji Erling Haaland, Mino Raiola amekanusha uvumi unaoenea kuwa amepokea Euro milioni 40 ambazo ni sawa na bilioni 108 na zaidi ya milioni 954 za kitanzania pamoja na baba wa mchezaji huyo Alfe-Inge Halaand kama sehemu ya makubaliano na Barcelona kumsajili Haaland.

Wakala wa Haaland, Mino Raiola (kushoto) na Haaland (kulia)

Raiola amekanusha kwa kuandika kwenye akaunti zake za mitando ya kijamii kuwa, Taarifa ambazo si za kweli husambaa mbali na haraka sana huku akiambatanisha na picha iliyokuwa ikielezwa akipokea malipo hayo ya kumhamisha Halaand kutoka Dortmund ya Ujerumani na kutua Barcelona.

Ikumbukwe kuwa, kwa mujibu wa jarida la michezo la AS lilithibitisha kuwa Raiola alitua nchini hispania siku chache zilizopita kukutana na rais wa Barcelona wa sasa Juan Laporta na baadaye wawakilishi wa klabu ya Real Madrid kujadili uwezekano wa usajili ya kinda huyo hatari kwa ufungaji

Haaland ambaye kwasasa ndiye kinara wa ufungaji kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya akiwa na mabao 10, amefunga jumla ya mabao 33 na kutengeneza mabao 8 kwenye michezo 32 aliyoichezea klabu yake ya Borussia Dortmund ya Ujerumani kwenye michuano yote msimu huu.