Polisi kujiuliza kwa Namungo

Jumatatu , 14th Sep , 2020

Ligi kuu soka Tanzania bara VPL inaendelea tena hii leo kwa mchezo mmoja, mchezo namba 18 kati ya Namungo FC ya mkoani Lindi dhidi ya Polisi Tanzania ya Moshi Kilimanjaro.

Mshambuliaji mpya wa Namungo Stephen Sey wakati akikamilisha usajili wake akitokea Singida United.

Katika Dimba la Majaliwa Luangwa mkoani Lindi majira ya saa 10 jioni klabu ya Namungu wanashuka Dimbani wakiwinda ushindi wa pili kwenye ligi kuu watakapo kuwa wanaminyana na Polisi Tanzania.

Mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa ligi Namungu waliibuka na ushindi wa bao 1- 0 dhidi ya Coastal Union bao pekee ambalo lilifungwa na mshambuliaji Blaise Bigirimana.

Mchezo wa kwanza Kocha Malale Hamsini wa Polisi kikosi chake kilianza vibaya kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Azam fc, mchezo uliochezwa katka dimmba la Azam Complex Jijini Dar es salaam. Huu ni mchezo wao wa pili ugenini Hivyo wanashuka dimba jioni ya leo wakiwa na malengo ya kupata walau alama yao ya kwanza msimu huu.

Kwenye msimamo Namungo wapo nafasi ya saba wakiwa na alama zao tatu, wakati Polisi wapo nafasi ya 15 na hawana alama hata moja.

Msimu uliopita Namungo walikusanya alama nne mbele ya Polisi, Namungo alishinda bao 1- 0 kwenye mchezo uliochezwa Lindi na wakaenda sare ya bila kufunga kwenye mchezo uliochezwa katika uwanja wa ushirika mjini Moshi.

.

MATOKEO YA JUMLA RAUNDI YA PILI

Gwambina 0-0 Kagera Sugar

Azam 2-0 Coastal Union

Jkt Tanzania 0-2 Dodoma Jiji

KMC 2-1 Prisons

Mtibwa Sugar 1-1 Simba

Biashara 1-0 Mwadui

Ihefu 1-0 Ruvu Shooting

Yanga 1-0 Mbeya City.

MSIMAMO 6 ZA JUU

KMC-6

AZAM-6

DODOMA JIJI-6

BIASHARA UTD-6

SIMBA -4

YANGA-4

MSIMAMO 4 ZA CHINI

15-POLISI TZ-0

16-MWADUI FC-0

17-COASTAL UNION-0

18MBEYA CITY-0