Jumamosi , 8th Jan , 2022

Nyota wa Japan anayetamba katika mchezo wa Tenisi, Naomi Osaka amepata majeraha ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza kwa mashindano ya Australian open yanayotarajia kutimua vumbi January 17.

Naomi Osaka

Osaka ambaye ndiye bingwa mtetezi wa Australian Open, alipata majeraha kwenye eneo la tumbo katika michezo ya maandalizi yanayoendelea mjini Melbourne huku akitanabaisha kuwa atarejea kabla ya michuano hiyo kutimua vumbi.

Osaka aliandika kwenye Twitter: "Inasikitisha kujiondoa kwenye za majaribio kutokana na jeraha kwenye mechi yangu ya leo, mwili wangu ulipata mshtuko kwa kucheza mechi kali za nyuma baada ya mapumziko niliyochukua. Nitajaribu kupumzika na nitakuona hivi karibuni! "

Bingwa huyo mara nne wa Grand Slam alichukua mapumziko ya muda usiojulikana baada ya kufungwa na Leylah Fernandez aliyefika fainali katika raundi ya tatu ya michuano ya US Open iliyofanyika Septemba.

Osaka - ambaye sasa anaorodheshwa katika nafasi ya 13 duniani kwenye mchezo wa Tenisi alisema lengo lake kuu la 2022 ni kuhakikisha anarudi kwenye ubora wake