Jumatano , 23rd Aug , 2017

Kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii  unaosubiriwa kwa hamu kati ya Simba dhidi ya Yanga leo saa 11 jioni katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, timu ya Simba SC imetoa kikosi chake kikiongozwa na Haruna Niyonzima pamoja Emmanuel Okwi.

 

Kupitia Msemaji wa Klabu hiyo Haji Manara amekiweka Kikosi hicho hadharani mapema wakati timu hiyo ikiwa tayari inaelekea uwanjani.

Kikosi cha Simba kinaongozwa na Kipa mpya akitokea Azam FC Aishi Manula  wachezaji wengine wakiwa ni

2.Ally Shomari

3.Erasto Nyoni

4.Salim Mbonde

5.Method Mwanjale

6.James Kotei

7.Shiza Kichuya

8.Mzamiru Yassin

9.Laudit Mavugo

10.Emanuel Okwi

11.Haruna Niyonzima

Pamoja na hao Kikosi cha wachezaji wa akiba ni pamoja na 1. E. Mseja 2.M. Tshabalala 3.Juuko M 4. J. Mkude 5.M.Kazimoto 6.J Luizio 7.MO Ibrahim