Ni kiwango tu, ndo kinamuweka Ozil Benchi

Ijumaa , 11th Sep , 2020

Mesut Ozil lazima afanye vizuri mazoezini na kwenye mechi anapopata nafasi ya kucheza ili aingie kwenye mipango ya kocha Mikel Arteta amesisitiza mkurugenzi wa ufundi wa Arsenal Edu.

Ozil lazima afanye vizuri mazoezini ili arejee kwenye kikosi cha kwanza amesema mkurugenzi wa ufundi wa Arsenal Edu.

Kabla ya mlipuko wa virusi vya Corona Ozili alikuwa akipata nafasi ya kucheza mara kwa mara chini ya kocha Arteta, lakini baada ya ligi kurejea tena kiungo huyu wa kimataifa wa Ujerumani hajacheza mchezo hata mmoja.

 

Mkurugenzi wa ufundi wa Arsenal Edu anasema hakuna kitu chochote cha ziada kinachomfanya Ozil akaosekane kwenye timu, na Mikel Arteta anatoa nafasi kwa wachezaji wanaofanya vizuri mazoezini na kwenye mechi.

 

Edu anasema 'tunajua umuhimu wa kila mmoja, najua ni muhimu kiasi gani na ni jina kubwa kiasi gani ukimtaja Mesut Ozil lakini mwisho wa siku tunaongelea bora. Kama anafanya vizuri , watu wanafanya vizuri, nani ni bora kwenye mazoezi, bora kwenye mchezo na uhakika Arteta atachagua''

 

Ozil amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake na klabu ya Arsenal, na ameweka wazi kuwa ataendelea kusalia klabu hapo. Kwa sasa kiungo huyu ndo mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa kwenye klabu hiyo akichukua pesa za Uingereza Pauni laki tatu na nusu kwa wiki.

 

Awali kulikuwa kuna ripoti kuwa klabu ya Arsenal inampango wa kumuuza Ozil ili kupunjguza bajeti ya mshahara kwenye klabu hiyo hasa baada ya uchumi kuyumba kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona amabao ulisababisha baadhi ya shughuli za kibiashara kwenye soka kusimama.

Arsenal watauanza msimu mpya wa 2020-21 wa ligi kuu England EPL Ugenini dhidi ya Fulham kesho septemba 12 katika dimba la Craven Cottage.