Jumanne , 21st Feb , 2017

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Yanga, Donald Dombo Ngoma hataweza kucheza mechi kati ya watani wa jadi kati ya Simba na Yanga kutokana na kuwa majeruhi.

Donald Ngoma

Donald Ngoma amesema hayo leo alipokuwa akichat live na mashabiki wake kupitia ukurasa wake wa facebook na kusema haweza kucheza mchezo huo wa watani wa jadi kutokana na kuwa na majeraha hivyo atakuwa nje ya uwanja. 

Ngoma anasema ameamua leo kuwapa taarifa mashabiki kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa wiki kadhaa na kusema watu wanaosema kuwa amegoma kucheza siyo wa kweli kwani yeye amekuja Tanzania kwa ajili ya kucheza mpira hivyo asipocheza itakuwa ni kama dharau, hivyo anadai sababu kubwa inayofanya ashindwe kucheza ni majeruhi na si kitu kingine.

Mbali na hilo Donald Ngoma amewataka mashabiki wa Yanga kutokuwa na wasiwasi yeye kutocheza mchezo wa Jumamosi kwani anadai anaamini Yanga ina wanajeshi wengi wapambanaji hivyo wataisaidia timu kupata matokeo mazuri.

"Timu yetu ina mashujaa wengi, yupo Msuva pale, Tabwe bila kumsahau Haruna, na wanajeshi wengine wa Yanga ambao wote ni wazuri hivyo mimi kukosekana haiwezi kuleta athari yoyote, unajua mpira ni mchezo wa kushirikiana hauchezwi na mtu mmoja, bali unachezwa na watu wengi kwa kutegemeana hivyo naamini Yanga itafanya vyema siku ya Jumamosi" alisema Donald Ngoma