Jumatano , 28th Jun , 2017

Mshambuliaji wa kimataifa raia wa Zimbabwe, Donald Dombo Ngoma amesaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwatumikia mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Young Africans.

Kwa hatua hiyo Ngoma anazizika zile tetesi zilizokuwa zimezagaa kwa kasi zikimuhisisha mshambuliaji huyo kusajiliwa na Klabu ya Polokwane ya nchini Afrika Kusini huku nyingine zikidai kusajiliwa na watani wao wa jadi, Simba Sc.

Katika msimu uliyopita wa Ligi kuu Ngoma alifanikiwa kufunga mabao 8 japokuwa hakuweza kuonekana mara kwa mara uwanjani kutokana na majeruhi yaliyokuwa yakimuandama. 

Ngoma akimwaga wino leo