Ijumaa , 16th Oct , 2020

Mchezaji mwandamizi wa Mtibwa Sugar Shaban Nditi amesema licha ya matokeo mabaya wanayoyapata kwenye michezo ya mwazo ya ligi kuu, kamwe hawawezi kushuka daraja,

Shaban Nditi akiwa kwenye moja ya mechi ya timu yake ya Mtibwa Sugar

 

Kauli ya Nditi imekuja baada ya timu hiyo kupoteza michezo 3 mfululizo, amesema haya kufuatia timu yake kukubali kichapo cha bao 2-0 toka kwa Biashara Mara,na nyuma walitoka kupoteza michezo miwili dhidi ya Gwambina na Yanga

Nditi alisema ''nikweli tunapitia changamoto ya matokeo ya mwisho wa mchezo lakini ndani ya uwanja tunacheza vizuri, ni kama upepo mbaya umetupitia, lakini ni suala la muda tu benchi la ufundi litarekebisha mapungufu na baada ya hapo tutaanza kupata matokeo''

''Hata msimu uliopita, tulipitia changamoto kadhaa, wengi wakaamini tutashuka daraja lakini mwisho wa msimu hatukushuka daraja''

Shaban Nditi ni moja ya wachezaji wazoefu katika ligi kuu Tanzania bara, amecheza kwa zaidi ya miaka 20 katika timu za ngazi ya klabu na timu ya Taifa, pia amedumu Mtibwa kwa zaidi ya miaka 18 ingawa  aliwahi kuhamia Simba 2006-2008