Mpango wa JKT mbele ya Simba SC

Jumatatu , 1st Mar , 2021

Ligi Kuu soka Tanzania bara itaendelea leo kwa mchezo mmoja ukiwa ni mzunguko wa 22 katika uwanja wa Benjamini Mkapa, mabingwa watetezi Simba SC watakuwa wenyeji wa JKT Tanzania ya Dodoma mchezo utapigwa majira ya Saa 1:00 usiku.

Ligi Kuu leo Simba Vs JKT Tanznaia

Simba wanaingia kwenye mchezo wa usiku wa leo wakiwa wanawazidi JKT Tanzania kwa tofauti ya alama 18, mabingwa hao watetezi wa VPL wekundu wa msimbazi ambao hawajapoteza mchezo hata mmoja kwenye michezo 5 ya mwisho ya Ligi kuu wakiwa wameshinda michezo 4 na sare mchezo 1, wapo nafasi ya pili wakiwa na alama 42, kwenye michezo 18.

JKT wamekusanya alama 24 kwenye michezi 21 wakiwa wanamiliki nafasi ya 10 kwenye msimamo, wameshinda michezo 3 kwenye michezo 5 ya mwisho ya ligi wamefungwa mchezo mmoja na wametoka sare mchezo mmoja.

Mchezo wa mkondo wa kwanza timu hizi zilipokutana mchezo ambao ulichezwa jijini Dodoma katika Dimba la Jamhuri Simba iliibuka na ushindi wa mabao 4-0, mabao ya Simba yalifungwa na Meddie Kagere ambaye alifunga mara mbili, mabao mengine yalifungwa na Chris Mugalu na Luiz Miquissone.

Kwenye michezo 5 ya mwisho timu hizi kukutana Simba wamekuwa na rekodi bora mbela ya JKT Tanzania kwani wameshinda michezo 4 na wamefungwa mchezo mmoja tu.