Jumanne , 14th Feb , 2017

Michezo miwili ya michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya katika hatua ya kumi na sita bora itachezwa leo nchini Ureno na Ufaransa.

Huko nchini Ureno Benfica watakuwa wenyeji wa Borussia Dortmund kutoka nchini Ujerumani mchezo utakaochezwa katika Uwanja wa Sport Lisboa de Benfica, na mwamuzi wa mchezo huo ni Nicola Rizzoli raia wa Italia.

Mchezo wa pili utawakutanisha Paris Saint Germain ya Ufaransa watakaokipiga na miamba wa Hispania Barcelona mchezo ukichezwa katika dimba la Parc des Princes jijini Paris.

Kesho, zitachezwa mechi nyingine mbili, Bayern Munich watachuana na Arsenal wakati Real Madrid watatunishiana misuli na Napoli ya Italia huku mechi nyingine nne za michuano hii ya Ulaya hatua ya 16 bora zitachezwa wiki ijayo.