Mkamia maji hayanywi,Zlatan kuwakosa Man United

Jumanne , 2nd Mar , 2021

Imethibitishwa kwamba mshambuliaji tegemezi wa timu ya AC Milan Zlatan Abrahimovic, atakosekana katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Europa, kutokana na majeraha aliyoyapata jumapili hii katika mchezo wa ligi kuu 'Serie A' walipocheza na AS Roma.

Zlatan Ibrahimovic ataikosa timu yake ya zamani Manchester United

Licha ya AC Milan kuibuka na ushindi wa 1-2 wakiwa ugenini, lakini mshambuliaji wao tegemezi Zlatan alipatwa na majeruhi yatakayomfanya akae nje kwa siku 10 hadi 14 , hivyo kuikosa timu yake ya zamani Manchester United katika mchezo wa mkondo wa kwanza unaotarajiwa kuchezwa tarehe Alhamis ya 11/03/2021.

Zlatan huenda akaukosa mchezo wa AC Milan dhidi ya Napoli unaotazamiwa kuchezwa tarehe 14 /03/2021 ukiwa ni mchezo wa ligi ya Italia maarufu kama 'Serie A'.

Endapo Zlatan Ibrahimovic akikosekana ndani ya kikosi cha AC Milan katika mchezo dhidi ya Manchester United, huenda wakapoteza mchezo huko kutoka na umuhimu na mchango wake kwa timu hiyo,

Zlatan amekuwa bora msimu huu ndani ya AC Milan amefunga goli 14 katika michezo 15 ukiwa ni msimu wa pili, na msimu uliopita alifunga magoli 10 katika michezo 18, alikosa michezo mingi kutokana na majeruhi.