Ijumaa , 8th Jan , 2021

Waziri wa Mambo ya Nje ya China, Wang Yi ametoa hundi ya shilingi milioni 350  kwa Chuo cha Veta  wilaya ya Chato, ili kuhakikisha  wanafunzi watakaosoma wanapata ujuzi wa  kutosha juu ya fani ya uvuvi wa samaki.

Waziri wa Mambo ya Nje ya China Wang Yi

Waziri Wang Yi, amekabidhi hundi ya kiasi hicho kwa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako , mara baada ya kuzindua chuo cha ufundi stadi wilayani humo.

Waziri wa Mambo ya Nje ya China, Wang Yi (wa pili kutoka kushoto), Waziri wa Elimu  Profesa Ndalichako (wa tatu kutoka kushoto) na Waziri wa Mambo ya Nje Prof. Paramagamba Kabudi (kulia).

Kwa Upande wake Profesa Ndalichako, amesema watatumia kiasi hicho kwa ajili ya kuendeleza fani ya uvuvi chuoni hapo.

“Katika chuo hiki tuna fani ya uvuvi kwahiyo msaada huu tutautumia kununua vifaa kwa ajili ya kuendeleza fani ya ufundi, wananchi wa chato wengi ni wavuvi”, amesema Ndalichako.

Zaidi tazama Video hapo chni