Ijumaa , 20th Nov , 2020

Ligi pendwa Duniani, Ligi kuu ya nchini Uingereza maarufu 'EPL' inatazamiwa kurejea kwa kishindo hapo kesho kwa michezo minne, baada ya kusimama kwa muda wa wiki mbili kupisha michezo mbalimbali ya timu za taifa ambazo zimetamatika usiku wa kuamkia jana.

Mshambuliaji wa Manchester City, Sergio AGuero(kushoto) akikatiza mbele ya kiungo wa Tottenham Hotspurs, Delle Ali (Katikati) na Eric Dier (Kulia) katika mchezo uliowakutanisha.

Vigogo Chelsea watakuwa ugenini kuchuana na Newcastle United saa 9:30 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki kwenye dimba la St.James lenye historia mbovu na Chelsea tokea mwaka 2004 ambapo The Blues wameshinda mchezo mmoja pekee, sare 2 na vipigo 3 kwenye michezo 5 ya mwisho ya EPL tu.

Kuelekea kwenye mchezo huo unataraji kuwa wa ushindani Chelsea akitaka kufuta uteja kwenye dimba la St.James, Chelsea wanatazamiwa kuwakosa wachezaji wake nyota Christian Pulisic na Kai Havertz ambao wanasumbuliwa na majeraha wakati Callum Wilson wa Newcastle akiwa fiti.

Kwa upande wa timu wenyeji klabu ya Newcastle Utd, Mshambuliaji wake wakutumainiwa Callum Wilson mwenye mabao 6 na kutengeza 1 kwenye michezo 7 anatarajiwa kuwepo dimbani.

Mara ya mwisho wawili hawa kukutana ilikuwa ni tarehe 18 mwezi januari mwaka huu ambapo Newcastle walipata ushindi wa bao 1-0 kwenye dimba lake la nyumbani kwenye mchezo wa EPL.

Vijana wa Dean Smith Klabu ya Aston Villa wanaoshika nafasi ya 6 kwenye msimamo wa EPL watachuana na Brighton and hove albion waliopo nafasi ya 16 mishale ya saa 12 kamili jioni kwa saa za Afrika ya Mashariki kwenye dimba la Villa park.

Mchezo unaosubiriwa na wapenzi wengi wa soka hapo kesho ni ule utakaowakutanisha Tottenham Hotspurs na Manchester City, ni vita nyingine kati ya kocha Jose Mourinho na Pep Guadiola ambaye jana ameongeza kandarasi ya miaka miwili na The Citizens hadi 2023.

Mchezo huo unatazamiwa kuwa wa kukata na shoka kutokana na Ubora wa Spurs msimu huu hadi hivi sasa kwa kushinda michezo 5, sare 2 na kufungwa mchezo 1 na kujizolea alama 17 alama moja nyuma ya kinara Leicester City ilhali Man City ni wa 10, ushindi michezo 3, sare 3 na kipigo 1 na alama 12.

Spurs ndiyo timu ya kwanza kufungwa mabao machache 9 na wapili kwa timu zenye mabao mengi 19 akizidiwa bao 1 na Chelsea wakati City ikifanana na Spurs kwenye kuruhusu mabao machache wakati ikiwa hafifu kwenye ufungaji ikiwa na mabao 10 pekee tofauti kubwa na msimu uliopita.

Manchester United dhidi ya West bromwich Albion ni mchezo mwingine wa EPL utakaopigwa hapo kesho wenyewe ukitazamiwa kuchezwa saa 5 mashetani wekundu imepoteza 3 na sare 1 na kushinda michezo 3 ugenini.

Kocha wa Man Utd Ole gunnar Solskjear ataendelea kuwa kwenye presha endapo ataendelea kutopata matokeo mazuri kwenye mchezo wa hii leo na kusaka ushindi wake wa kwanza kwenye dimba la Old Trafford tokea EPL inaanze msimu huu.