Masau Bwire aja na 'slogan' mpya kwa wapinzani

Jumapili , 13th Sep , 2020

Msemaji wa wababe wa Mlandizi Pwani Ruvu Shooting Masau Bwire baada ya kutamba msimu uliopita na msemo wake maarufu 'mpapaso square' msimu huu Masau Bwire amekuja na msemo mpya.

Msemaji wa wababe wa Mlandizi Pwani Ruvu Shooting Masau Bwire

Masau Bwire ameweka wazi msemo huo utakaotumika msimu huu wa 2020-21 utakuwa ni 'kupapasa na kukung'uta'.

"Kama ambavyo watanzania wanavyotutambua kuwa sisi ni 'Barcelona ya bongo' hivyo wapinzani wetu wajiandae maana tutawapapasa na kuwakung'uka'', amesema Masau.

Aidha, kwa upande mwingine Masau Bwire amezungumzia usajili walioufanya na maandalizi yao katika mashindano yote msimu huu 2020-21 kuwa ni usajili wa kitaalamu zaidi uliozingatia thamani na vipaji walivyonavyo wachezaji wazawa

"Tofauti yetu na vilabu vingine vinavyosajili kwa mbwembwe sisi tunamini katika vipaji vya wazawa hata hivyo niwaase tu timu zinazosajili wachezaji wakigeni, nyumbani tunawachezaji bora zaidi. Laiti kama hizi fedha wanazopewa wachezaji wakigeni wangeboreshewa maisha wachezaji wazawa naaminin wachezaji wazawa ni bora zaidi na hii ndiyo Ruvu Shooting tunaenda kuwadhihirishia'', ameongeza.