Jumamosi , 27th Mei , 2017

Kipa Bora wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara msimu huu na nyota wa Azam FC, Aishi Manula, amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kufuatia taarifa zinazoenezwa kuwa tayari amesaini Simba kwa ajili ya kuitumikia kwa msimu ujao.

Mlinda Mlango wa Azam FC, Aishi Salum Manula

Manula amesema bado ana mkataba na Azam FC utakaomalizika Julai mwaka huu, na hivi sasa yupo kwenye mazungumzo na viongozi wa Azam FC juu ya kuuongeza.

Kipa huyo namba moja wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, ameweka wazi kuwa mazungumzo hayo yanaendelea vizuri na anaamini atasaini katika timu hiyo iliyomtunza na kumlea vema hadi leo hii kuanzia kwenye academy yake hadi timu kubwa.