Jumatatu , 20th Sep , 2021

Bondia wa kimataifa kutoka nchini Ufilipino, Manny Pacquiao ameweka wazi dhamira yake ya kuwania nafasi ya kiti cha urais kwa mwaka 2022, kwa kutokupendezwa na ufisadi uliokithiri kwenye serikali iliyopo madarakani chini ya Rais Rodrigo Duterte ambaye anayemaliza wakati wake.

Bondia Manny Pacquiao akizipiga na Yordenis Ugas wa Cuba kwenye mpambano wa kuwania mkanda wa ubingwa wa WBA super welterweight Agosti mwaka huu ambapo Pacquiao alipigwa na kupotwza ubingwa huo.

Pacquiao, ambaye sasa ni seneta, aliteuliwa Jumapili na washirika wake wa chama cha PDP-Laban wakati wa bunge la kitaifa la chama hicho, ikiwa ni siku chache baada ya chama tawala kumchagua Rais wa sasa kama chaguo lao kuwania nafasi ya makamu wa urais na msaidizi wake wa muda mrefu, Seneta Christopher Go, kama mgombea urais.

Pacquiao kwa nyakati tofauti alikuwa mshirika wa karibu wa Rais Duterte, lakini baada ya uchuguzi wake na kugundua kuwa zaidi ya bilioni 10 za kifilipino zilizotolewa kwaajili ya misaada ya janga la UVIKO-19 iliyokusudiwa kusaidia familia masikini bado hazijulikani zilipokwenda.

Bingwa huyo wa mara nane kwenye uzani wa kati wa ngumi ulimwengu na shujaa mpendwa wa kitaifa anamaliza uvumi uliokuwa ukiendelea juu ya kustaafu masumbwi wiki kadhaa baada ya kupoteza pambano lake la mwisho la dhidi ya Mcuba, Yordenis Ugas huko Las Vegas.