Alhamisi , 29th Sep , 2022

Afisa Habari wa Yanga Ally Kamwe ameweka wazi kuwa baada ya kutangazwa rasmi kwenye idara ya habari na mawasiliano alipongezwa na Haji Manara ambaye ni msemaji wa Yanga.

Ofisa Habari wa Yanga Ally Kamwe

Septemba 27, Kamwe alitangazwa kuwa Afisa Habari na Priva Abiud maarufu kama Privaldinho alitangazwa kuwa Msimamizi Mkuu wa Digital na Maudhui.

Akizungumza na waandishi habari , Kamwe amesema kuwa alijisikia kuwa mwenye furaha baada ya kutangazwa kuanza majukumu mapya huku akiomba ushirikiano kwa mashabiki wa Yanga .

“Baada ya kutangazwa nimepewa pongezi nyingi ikiwa ni pamoja na kutoka kwa Haji Manara na Ahmed Ally, meneja wa kitengo cha habari na mawasiliano ndani ya Simba wote wamefurahi mimi kutangazwa.

“Nilifurahi nilipopewa taarifa hizi kwa kuwa mimi ni shabiki wa Yanga na kazi kubwa ambayo nitafanya ni kushirikiana na wengine ili kufikia malengo yetu,” amesema  Kamwe.

Oktoba 3 mwaka huu kikosi cha Yanga kinajitupa katika   uwanja wa Benjamin Mkapa kwenye muendelezo wa ligi hiyo itakapoivaana Ruvu Shooting .