Kundi la Namungo Kombe la shirikisho lajulikana

Jumatatu , 22nd Feb , 2021

Klabu ya soka ya Namungo imepangwa katika kundi D la kombe la shirikisho endapo itafuzu hatua hiyo, kufuatia Shirikisho wa soka la Africa CAF kupanga droo ya makundi hayo leo.

Wachezaji wa Namungo wakishangilia moja ya magoli yao

Namungo au CD Agosto mshindi kati yao ataenda kuingia na kundi D lenye timu za Raja Casablanca ya Morocco, Pyramids Misri na Nkana ya Zambia.

Namungo ipo kwenye mazingira mazuri zaidi ya kufuzu hatua hiyo, baada ya kushinda mchezo wake wa kwanza 2-6 dhidi ya CD Agosto ya Angola, mchezo uliyochezwa jana Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar-es-salaam, kufuatia shirikisho la soka Africa CAF kuamuru mechi zote mbili kuchezwa Tanzania

Awali kulikuwa na sintofahamu kufuatia mchezo wa kwanza kushindwa kufanyika kule Angola kwa sababu ya kanuni za kuthibiti janga la Corona hasa baada ya wachezaji 3 na kiongozi moja toka Namungo kudaiwa kukutwa na maambukizo hayo

CAF wamelazimika kupanga makundi hayo bila kujali kama mechi za mzunguko wa 32 zimemalizika hivyo basi mshindi wa jumla katika mchezo wa Namungo na CD Agosto ataenda kuungana na kundi D.