Kuhusu mgawanyiko ndani ya Man United

Ijumaa , 16th Oct , 2020

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anaamini watu wa nje wanajaribu kuunda mgawanyiko klabuni kufuatia ripoti kwamba kiungo wa kati Bruno Fernandes alikuwa amepoteza imani na meneja wake.

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solksjear (Kushoto) akiwa na Bruno Fernandes alipokua akisaini mkataba wa kujiunga na mashetani wekundu.

Ripoti ziliibuka wakati wa mapumziko ya kimataifa zikidai Fernandes hakufurahishwa na Solskjaer alipomuondoa baada ya kipigo cha nyumbani cha 6-1 dhidi ya Tottenham kwenye Ligi ya ya England

Baada ya taarifa hizo Solksjear alisema"Tunajua kuna baadhi ya watu nje ya klabu wakipata nafasi wanataka kuunda mgawanyiko.

Nadhani Bruno alizungumza vizuri siku alipohojiw.Tumeungana na tunapaswa kukaa pamoja ". Hatuwezi kusikiliza kila mtu aliye nje, lazima tuendelee na mipango yetu. ''

Hata hivyo Fernandes ambaye aliulizwa swali hilo akiwa katika timu yake ya taifa ya Ureno, alikuwa mwepesi kuzima mazungumzo yoyote ya mgawanyiko kati yake na meneja wake akisema hadithi hizo ziliundwa ili kudhoofisha umoja uliopo.

Solskjaer alifurahishwa na majibu ya kiungo wake, ambaye alisajiliwa kutoka Sporting Lisbon mnamo Januari, na kumwambia akaribie Manchester United, hiki ndicho kinachotokea pindi ambapo timu inapoteza.