Kiungo Cesc fabregas aandika rekodi yake

Jumatatu , 14th Sep , 2020

Cesc Fabregas afikisha mechi 800 tangu aanze kucheza soka la ushindani 2003 akiwa na umri wa miaka 16 alipojiunga na Arsenal lakini rekodi hii ameiweka akiwa na timu ya Monaco ambapo idadi hii ya mechi inahusisha mechi za ngazi ya klabu na timu ya Taifa

Cesc fabregas anayekipiga kwa sasa Monaco

Si jambo rahisi kwa mchezaji kufikisha mechi nyingi kwa kiasi hichi kwa mchezaji aliyecheza chini ya miaka 20 katika maisha  ya soka, Fabregas amefikisha mechi hizo katika mchezo wa mwishoni mwa wiki kati ya timu yake Monaco na Nantes iliyoisa kwa ushindi wa  2-1,lakini hizo mechi zimepatikana katika timu 4 alizopita katika ngazi ya klab ikiwemo  Arsenal, Barcelona na  Chelsea na sasa  Monaco na Timu ya Taifa

Fabregas  zao la akademi ya Barcelona ( La Mesia) akiwa pamoja na lionel Messi  ni moja ya  wachezaji wenye uwezo mkubwa kiuchezaji akicheza kwenye nafasi ya kiungo mshambuliaji. Pamoja na ushindani alioukuta kwenye  timu ya Arsenal  kwenye nafasi yake hasa alipokuwepo   Patrick  Viera ilimchukua muda mchache  kupata nafasi na kuwa   muhimu katika timu

Hata pia kwa upande wa timu ya Taifa ya Spain alipata upinzani wa nafasi ya moja kwa moja kwa wachezaji wenzie  aliokuwa nao pale La Masia kama Xavi Harnandez  na  Andreas Iniesta

MECHI HIZO  800 ZIMEPATIKANA KWENYE TIMU 4 KWA  UWIANO HUU

Arsenal  303

Barcelona 151

Chelsea  198

Spain      38

Pamoja na kushinda vikombe kadhaa akiwa ikiwemo kombe la Ulaya 2008  ,2012 na pia   kombe la dunia  2010  Afrika kusini  , kwa ngazi ya club ametwa vikombe vingi kwa ligi mbalimbali alizoshiriki