Alhamisi , 16th Feb , 2017

Mbunge wa Chalinze ambaye pia ni miongoni mwa wadau wakubwa wa soka nchini Tanzania, Ridhiwani Kikwete ameutaka uongozi wa klabu ya FC Barcelona ya nchini Hispania kurudi kwenye falsafa yake ya uchezaji, na kuachana na mtindo unaotumiwa hivi sasa.

Ridhiwani Kikwete

Kikwete ametoa taarifa hiyo ya kuwasiliana na uongozi wa Barcelona jana akiwa kwenye kipindi cha East Africa Breakfast cha EA Radio, ambapo amesema kuwa yeye kama mwanachama wa klabu hiyo ameumizwa sana na matokeo mabaya iliyopata klabu hiyo juzi dhidi ya PSG, akidai kuwa sababu kubwa ya matokeo hayo ni kocha wa Barcelona Luis Enrique kuachana na falsafa ya 'tic-tac'.

Amesema mara baada ya kushuhudia timu hiyo ikichapwa mabao 4-0 na PSG katika michuano ya Mabingwa Ulaya, aliamua kuuandikia uongozi wa timu hiyo ujumbe 'MEMO' akitoa ushauri wake kwa kuwa yeye ni mwanachana anayetambulika klabuni hapo na si shabiki wa kawaida.

Msikilize hapa Kikwete akifafanua............................

Mechi ambayo Barcelona imepigwa 4-0 na PSG