Jumanne , 23rd Feb , 2021

Timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 maarufu kama 'Ngorongoro heroes 'iliyokuwa inashiriki mashindano ya AFCON Mauritania imetolewa.

Kocha wa Ngorongoro heroes Jamuhuri Kihwelo 'Julio'

Ngorongoro heroes ilikubali kichapo cha bao 3-0 toka kwa timu ya taifa ya Morocco katika mchezo wa jumatatu usiku, na kukamilisha ushiriki wake baada ya michezo mitatu ikimaliza na point 1 kibindoni .

Mechi hii ilikuwa kipimo kingine kwa kocha Jamuhuri Kihwelo 'Julio', ambapo uteuzi wake ulileta mjadala mkubwa sana toka kwa wadau wa mchezo huu nchini Tanzania,juu ya uwezo wake na mahitaji katika soka la kisasa.

Katika mchezo wa jana Ngorongoro heroes iliuanza mchezo taratibu kwa makosa ya hapa na pale na kujikuta wanafanya madhambi yaliyosababisha penati dakika ya 4' tu, na baadaye ndani ya dakika 20 ikaruhusu jumla ya mabao matatu.

Kiufundi timu haikuzidiwa sana, woga na makosa ya haraka ndiyo yaliyowapa Morocco kupata magoli hayo ya haraka hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Ngorongoro wapo nyuma bao 3, lakini kipindi cha pili walianza kuimarika kadri muda unavyoenda na hatimaye mchezo kumalizika kwa kupoteza kwa 3-0.

Ngorongoro heroes imemaliza mashindano haya ikiwa na alama 1, katika michezo 3 iliyoshuka dimbani akiwa wamefungwa magoli 8 huku wao akipata goli 1, walipoteza 4-0 kwa Ghana, wakatoka 1-1 na Gambia na mchezo wa mwisho kupoteza kwa 3-0 dhidi ya Morocco