Jumatatu , 3rd Nov , 2014

Kocha wa timu ya walemavu ya mchezo wa Tenis, Riziki Salum ameomba wadau mbalimbali wa mchezo huo kujitokeza kwa ajili ya kusaidia timu hiyo ili kuweza kushiriki mashindano mbalimbali yakiwemo yanayotarajiwa kufanyika Desemba 13 mpaka 14 mwaka huu.

Akizungumza na East Africa Radio, Riziki amesema mchezo huo unahitaji gharama hususani kwa watu wenye ulemavu ambao wanahitaji vifaa kwa ajili ya kuwasaidia kutokana na hali waliyonayo ambapo wanahitaji kupata usafiri wa kuwapeleka na kuwarudisha mazoezini.

Riziki amesema jamii inatakiwa kujitokeza ili kuweza kuisaidia timu hiyo ambayo bado inahitaji msaada zaidi ili kuweza kufanya vizuri zaidi ya hapo ilipo hivi sasa.