Jadon Sancho awekwa sokoni

Jumatatu , 5th Apr , 2021

Mtendaji mkuu wa klabu ya Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke amesema watamuuza winga wao Jadon Sancho endapo kama kuna timu italeta ofa ya kutaka kumnunu mchezaji huyo, winga huyo raia wa Uingereza anatajwa kuwa na thamani ya pauni milioni 110.

Jadon Sancho

Msimu uliopita klabu ya Manchester United ilikaribia kumsajiri Jadon Sancho, na winga huyo amekuwa akihusishwa sana kuihama Dortmund. Kutokana na kuporomoka kwa uchumi wa klabu hiyo Hans-Joachim Watzke ameweka wazi kuwa wapo tayari kumuuza mchezaji huyo.

 

"Sijishughulishi na ubashiri, sio vizuri. Jadon Sancho amekuwa nasi muda mrefu sana kuliko Erling Haaland, itabidi tuzungumze na Jadon pia.''

''Ikiwa kuna ofa ya kipekee tutaijadili na mchezaji na wakala kama kawaida. Walakini, nina hakika kwamba soko la usajili litaendeshwa kwa thamani ndogo sana msimu huu kipindi cha majira ya joto. Hususani kwa vilabu vikubwa unaweza kuona vidonda vilivyoachwa na Corona, na sio vidogo vya kutibu ndani ya wiki mbili.' amesema Hans-Joachim Watzke

Thamani ya Sancho sokoni inatajwa kuwa ni pauni milioni 110 ambayo ni zaidi ya bilioni 354 kwa pesa za kitanznaia. Dau ambalo Manchester United waligoma kulipa kwenye dirisha la usajili lilopita, Jadon mwenye umri wa miaka 21 amefunga mabao 12 msimu huu kwenye michezo 31 kweye mashindano yote.