Alhamisi , 8th Apr , 2021

Klabu ya Inter Milan inakaribia kutwaa ubingwa wake wa kwanza wa ligi kuu ya Italia tangu mwaka 2010,baada ya usiku wa kuamkia leo kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Sassoulo.

Mfungaji bora wa pili katika Serie A, Romelu Lukaku akishangilia bao lake la 20 msimu huu.

Mabao ya Inter Milan yalifungwa na Romelu Lukaku na Lautaro Martinez huku la kufutia machozi kwa Sassoulo lilifungwa na Hamed Traole.

Romelu Lukaku alifikisha bao la 21 katika mechi 28 pamoja na pasi za usaidizi wa mabao 9 na kumfanya awe mfungaji bora wa nne katika ligi tano bora Ulaya.

Ushindi huo umewafanya vijana wa kocha Antonio Conte kufikisha alama 71 baada ya michezo 29, huku ikiziacha majirani zao AC Milan wenye alama 60 huku Juventus wakiwa na alama tatu wenye alama 59.

Juventus iliibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Napoli, mabao yaliyofungwa na Cristiano Ronaldo na Paulo Dyabala huku bao la wageni likipachikwa kambani na Lorenzo Insigne kwa mkwaju wa penati.

Ushindi huo wa kikosi cha kocha Andrea Pirlo umewasogeza katika msimamo wa Serie A, wakiwa nafasi ya tatu kwa tofauti ya alama moja na AC Mialan, ingawa wana tofauti ya alama 12 na vinara Inter Milan.