Jumatatu , 12th Feb , 2024

Imechukua miezi minne na siku 8 Ihefu kupata ushindi wa Ligikuu tangu walivyo ifunga Yanga 2-1 October 4 2023.

Klabu ya soka ya Ihefu yenye Makazi Yake Jijini Mbeya imejikuta ikipitia katika kipindi  kigumu baada ya kucheza zaidi ya mechi 7 pasi kuambulia ladha ya Ushindi 

Ihefu hii Leo imeshinda 3-2 ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar huku mabao Yao yakifungwa na wachezaji wapya waliosajiliwa katika dirisha dogo la mwezi January kutokea Singida Fountain Gate FC

Mabao mawili ya Ihefu yaliwekwa kimiani kipindi cha kwanza na Marouf Tchakei na Duke Abuya wakati lile la ushindi lilifungwa kipindi cha pil cha mchezo na Elvis Rupiah