Huu hapa Mpango wa Simba SC dhidi ya Al Merrick

Jumatano , 3rd Mar , 2021

Klabu ya Simba SC imetangaza kikosi cha wachezaji 25 watakao safiri kueleka nchini Sudan leo, tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Al Merrikh utakao chezwa Jumamosi Machi 6, 2021. Mchezaji Bernard Morrison hajajumuishwa kwenye kikosi kinachosafiri.

Kikosi cha Simba SC

Kikosi hicho cha mabingwa wa Tanznaia bara na wawakilishi wa nchi kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika kitaondoka nchini leo majaira ya Saa 10:45 Jioni kuelekea Khartoum Sudan. Simba itashuka ugenini dhidi ya wenyeji wao AL Merrick , ikiwa ni michezo ya raoundi ya tatu ya kundi A, kundi ambalo Simba SC ndio kinara mpaka sasa wakiwa na alama 6 wakati Al Merrick wanaburuza mkia wakiwa hawana alama hata moja.

 

Mshambuliaji Bernard Morrison, Junior Lokosa, kiungo Said Ndemla na beki Ibrahim Ame ni wachezaji ambao wameachwa kwenye orodha ya wacheza watakao safari leo kwenda Sudan.

 

Hiki hapa kikosi kamili cha wachezaji 25 wa Simba kinachoondoka leo