Hebu fahamu Namungo walivyoichukulia poa Yanga

Alhamisi , 19th Nov , 2020

Uongozi wa klabu ya soka ya Namungo umesema hauna hofu ya kuondoka kwa aliyekuwa kocha wao Hitimana Thiery katika nyakati ambazo wanakabilia na mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Yanga utakaochezwa Novemba 22 mwaka huu.

Kocha Hitimana Thiery aliyeondolewa Namungo baada ya mkataba wake kumalizika.

Afisa Habari wa Namungo, Kindamba namlia ameiambia East Africa Radio kwamba timu yao inaweza kufundishwa na hata nahodha katika kipindi hiki kwakuwa wanaijua falsafa yao hivyo wataikabili Yanga na hata Al Rabita bila mashaka yoyote.

''Sisi hatuna hofu yoyote, hata nahodha au mchezaji yoyote anaweza kusimamia mazoezi na tukafanya vizuri. Kuhusu Hitimana Thiery anaondoka kama alivyokuja, hatukuweka hadharani makubaliano yetu  na leo hatusemi chochote hivyo tumeshamalizana nae na tunasonga mbele'' alisema Kindamba.

Katika hatua nyingine klabu hiyo inatarajiwa kumtambulisha Hemed Morocco kuchukua mikoba ya Hitimana Thiery ambaye mkataba wake na Namungo ulimalizika.