Jumapili , 19th Nov , 2017

Daud Goffin leo anatarajiwa kukabiliana na Grigor Dimitrov kwenye hatua ya fainali ya ATP baada ya kumtupa nje bingwa mara sita wa michuano hiyo Roger Federer.

Goffin raia wa Ubelgiji mwenye miaka 26, alitoka nyuma kwa seti 2-6 na kushinda 6-3 6-4 dhidi ya Mswis Federer.

Goffin amesema anajisikia furaha kubwa kushinda kwa mara ya kwanza mbele ya Federer ambaye amekutana naye mara sita na kupoteza mechi zote kabla ya hii ya saba ambayo ameshinda katika nusu fainali ya ATP.

Kwa upande wake Grigor Dimitrov alitinga fainali baada ya kumwondoa Jack Sock wa Marekani kwa seti 4-6 6-0 6-3 katika nusu fainali.

Hii inakuwa mara ya pili kwa Dimitrov na Goffin kukutana katika michuano hii ambapo katika mchezo wa kwanza hatua ya makundi uliofanyika jumatano wiki hii Goffin alishinda kwa seti 6-0 6-2.