Haikuwa rahisi kihivyo, Namungo yafuzu makundi

Ijumaa , 26th Feb , 2021

Klabu ya soka ya Namungo kutoka Ruangwa Lindi jana ilifuzu rasmi kushiriki hatua ya makundi kwenye kombe la shirikisho la CAF, baada ya kuwatoa CD de Agosto ya Angola kwa jumla ya magoli 7-5.

Kikosi cha Namungo ya Lindi kilichofuzu kucheza hatua ya makundi kombe la shirikisho la CAF

Namungo licha ya kupoteza mchezo wa jana kwa magoli 3-1, walinufaika na matokeo ya mkondo wa kwanza walipofanikiwa kushinda 6-2. katika mchezo uliochezwa pia katika uwanja huo huo wa Chamazi, ambapo kikanuni CD de Agosto walikuwa nyumbani.

Katika mchezo wa jana Namungo walionekana kuhitaji kurudia mafanikio yao ya mchezo wa kwanza kwa kupata bao la mapema dakika ya 7, bao lililofungwa mchezaji wake nyota Sixtus Sabilo, lakini kadri muda ulivyokuwa unakwenda wakapoteza umakini na kujikuta wanafungwa magoli 3-1.

Namungo baada ya kufuzu makundi ya shirikisho wamepangwa kundi D lenye timu za Raja Casablanca ya Morocco, Pyramids ya Misri pamoja na Nkana red Devils ya Zambia na mashindano yao yanatarajia kuanza tarehe 10/03/2021.