Jumatano , 3rd Mar , 2021

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amesema anajivunia kiwango bora cha timu yake lakini amekitahadharisha kikosi chake kuwa wamahitaji muendelezo wakupata matokeo mazuri ili wakusanye alama nyingi zaidi na kumpora ubingwa, bingwa mtetezi klabu ya Liverpool.

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola.

Guardiola ameyasema hayo baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Wolverhampton kwenye mchezo wa ligi kuu England uliochezwa usiku wa jana kwenye uwanja wa nyumbani wa Manchester City, uwanja wa Etihad.

Mabao ya City yamefungwa na Leander Dendoncker aliyejifunga dakika ya 15 kabla ya nahodha wake, Conor Coady kusawazisha dakika ya 61 ya mchezo. Licha ya vijana hao wa Espirito Santo kuonekana kuwamuda City, Lakini Gabriel Jesus alifanikiwa kufunga mabao mawili na Riyad Mahrez akifunga moja ndani ya dk 10 kabla mchezo kumalizika.

Baada ya ushindi huo, Manchester City wameweka rekodi ya kuwa timu pekee kupata ushindi kwenye michezo 15 mfululizo ya EPL msimu huu, huku ikifikisha ushindi wake wa michezo 21 mfululizo kenye michuano yote.

Manchester City imesalia kileleni mwa msimamo wa EPL ikiwa na alama 65 baada michezo 27, ikiwa ni alama 15 zaidi ya mtani wake wa jadi, klabu ya Manchester United inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 50 licha ya kuwa nyuma kwa mchezo mmoja.