Golden State Warriors yapata pigo la Klay Thompson

Ijumaa , 20th Nov , 2020

Mlinzi nyota wa timu ya mpira wa kikapu ya Golden State Warriors, Klay Thompson imethibitika atakosa michezo yote ya msimu mzima ujao wa NBA mwaka 2020-21 kwasababu ya kupata majeraha kwenye mguu wake wa kushoto akiwa anafanya mazoezi kusini mwa jiji la Kalifonia nchini marekani.

Nyota wa Golden State Warriors , Klay Thompson (Pichani chini) akiugulia maumivu alipoumia uwanjani.

Hii ni mara ya pili kwa Thompson mwenye umri wa miaka 30 kupata majeraha yatakayomuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu baada ya awali kupata maumivu ya goti kwenye mguu wake wa kushoto kwenye mchezo wa fainali ya NBA dhidi ya Toronto Raptors mwezi wa sita mwaka jana.

Kuumia kwa Klay Thompson kumewashtua wapenzi wa Golden State warriors ambao wanakumbuka msimu uliopita haukuwa mzuri sana kwao kutokana na kuumia kwake na kutocheza michezo pamoja na nyota wao mwingine Stephen Curry.