Alhamisi , 12th Jan , 2017

Wachezaji wa Arsenal, Olivier Giroud, Laurent Koscielny na Francois Coquelin wameongeza mikataba yao na klabu hiyo ya Ligi Kuu ya soka nchini Uingereza.

Wachezaji hao baada ya kusaini mikataba mipya

 

Arsenal haijatoa muda wa mikataba ya wachezaji hao wa Kifaransa, lakini beki Koscielny aliandika kwenye mtandao wa Twita kuwa ataitumia the Gunners hadi 2020.

Wafaransa hao wote watatu wamekuwa nguzo muhimu kwa Arsenal kwa sasa, ambapo Giroud amekuwa gumzo kwa kufunga mabao manne katika michezo minne iliyopita, kujumuisha na bao la kiufundi 'Scorpion Goal' alilofunga hivi karibuni kwenye mchezo dhidi ya Crystal Palace.